KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, November 23, 2009

BECKS AJIBEMBELEZA.


Gwiji wa soka toka nchini Uingereza na klabu ya LA Galaxy David Beckham amesema ataendelea kujivunia kuichezea klabu hiyo ya nchini Marekali licha ya usiku wa kuamkia leo kukosa mkwaju wa penati.

Kiungo huyo amekosa mkwaju huo wa penati kwenye mchezo wa hatua ya fainali ya ligi kuu ya soka nchini Marekani dhidi ya Real Salt Lake ambao waliibuka vinara kwa penati 5 kwa 4.

Hatua ya kupiga mikwaju hiyo ilifikiwa baada ya timu hizo kufungana bao moja kwa moja ndani ya muda wa dakika 120.

Akizungumza na vyombo vya habari Beckham amesema inamuuma kufanya vibaya katika mchezo huo lakini hatajutia kuichezea klabu hiyo ambayo ilimsajili mwaka 2007 akitokea Real Madrid akiwa kama mchezaji huru.

1 comment:

  1. Huyu mzee naye si angekataa nakaumpa mchezaji mwingine?Yani yeye kwakukosa penati ndani ya fainal ni namba moja,,hakubali kuzeeka?acheze tu mpila wakawaida penati awape walio na misuli mipya.

    ReplyDelete