KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, November 26, 2009

BENITEZ AMESALIMIKA.


Licha ya kuondioshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, uongozi wa klabu ya Liverpool umetoa tamko la kuendelea na meneja wa sasa wa kikosi chao Rafael Benitez.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Liverpool mkurugenzi mkuu wa Liverpool Christian Purslow amesisitiza nafasi ya Rafael Benitez bado itaendelea kuwepo na wanaamini meneja huyo ni madhubuti katika muhimili wa klabu yao.

Liverpool imeshindwa kusonga mbele kwenye hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita iliyopita, licha ya kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya klabu ya Debrecen.

No comments:

Post a Comment