Kiungo wa kimataifa toka nchini Cameroon Alexandre Song amekubali kusaini mkataba wa muda mrefu na klabu yake ya sasa ya huko jijini London Arsenal FC.
Kiungo huyo ambae kwa sasa ni msaada mkubwa katika kikosi cha Arsene Wenger, amesaini mkataba huo ambao utaendelea kumuweka huko Ashburton Grove hadi mwaka 2014.
Kiungo huyo ambae kwa sasa ni msaada mkubwa katika kikosi cha Arsene Wenger, amesaini mkataba huo ambao utaendelea kumuweka huko Ashburton Grove hadi mwaka 2014.
Song, ambaye aliwahi kupelekwa Charlton kucheza kwa mkopo mwaka 2007, alinunuliwa kwa pauni milioni moja kutoka timu ya Bastia mwaka 2006.
Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameeleza kwamba ni furaha kubwa kuendelea kuwa na mchezaji kama Song na ana imani kiungo huyo ataendelea kuitumikia klabu hiyo kwa moyo wake wote na kufikia malengo ya kutwaa vikombe vya michuano mbali mbali wanayoshiriki msimu huu.
No comments:
Post a Comment