KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, November 9, 2009

BENT KIKOSINI.


Mshambuliaji wa klabu ya Sunderland Darren Bent ameitwa katika kikosi cha wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza kitakachopambana na Brazil mnamo Novemba 14 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.


Bent, ambaye hadi sasa amepachika mabao manane katika Ligi Kuu ya soka nchini Uingereza anatarajiwa kung'ara kutokana na kukosekana kwa Emile Heskey ambaye ni majeruhi.


Wachezaji wengine walioitwa katika kikosi hicho cha Fabio Capello ni pamoja na beki wa klabu ya Aston Villa Stephen Warnock na kiungo wa klabu ya Tottenham Tom Huddlestone.


Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Uingereza dhidi ya Brazil unatarajiwa kupigwa nchini Qatar.


Mchezo huo utakuwa wa mwisho kabla Capello hajataja kikosi chake cha awali kwa ajili ya fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Afrika kusini mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment