Klabu ya Chelsea imeendeleza ubabe mbele ya klabu ya Fc Porto ambayo kwa muda mrefu imekua ngumu kufungika nyumbani pale inapocheza na klabu toka nchini Uingereza.Chelsea jana walikua huko Estadio Dragao wakicheza na wenyeji wao Fc Porto na kufanikiwa kupachika msimari mmoja ambao uligongelewa ubaoni na mshambuliaji wao wa kimataifa toka nchini Ufaransa Nicolas Anelka.
Kufuatia ushindi huo wa bao moja kwa sifuri Chelsea wamefikisha point 13 katika msimamo wa kundi la nne ambapo point hizo zinawapelekea moja kwa moje kwenya hatua ya 16 bora.

Mshetani wekundu Man Utd usiku wa kuamkia leo walilazimika kuvunja mwiko wa kutofungwa nyumbani kwao Old Trafford kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kukubali kisago cha bao moja kwa sifuri toka kwa Besiktas yanchini Uturuki.
Balo hilo ambalo limemaliza ukame wa kutokufungwa kwa Man Utd wakiwa nyumbani kwenye michuano hiyo ya Ulaya limefungwa na Rodrigo Tello katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza.
Hata hivyo pamoja na kuvunjwa kwa mwiko huo tayari Man Utd wameshajihakikishia nafasi ya kucheza 16 bora za michuano hiyo ambayo msimu huu inatarajiwa kuwa na upinzani mkali.

michezo mingine ya michuano hiyo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia leo ni pamoja na;
AC Milan 1-1 Marseille
Apoel Nicosia 1-1 Atletico Madrid
Bayern Munich 1-0 Maccabi Haifa
Bordeaux 2-0 Juventus
CSKA Moscow 2-1 Wolfsburg
Real Madrid 1-0 FC Zurich
No comments:
Post a Comment