













Penati ya utata iliyopatikana katika mazingira ya ndivyo sivyo na kupigwa na nahodha na kiungo wa wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard ilikiokoa kikosi cha Rafael Benitez mbele ya klabu ya Birmingham City iliyokuwa inaongoza kwa mbao mawili kwa moja kwa kipindi kirefu.
Gerrard alikwamisha wavuni penati hiyo baada ya David Ngog kumuongopea muamuzi Peter Walton wa kwa kujiangusha eneo la hatari wakati Lee Carsely akiwa katika harakati za kuutoa nje mpira ambao ungeleta madhara langoni mwao.
Hata hivyo katika mchezo huo Liverpool ndio walikuwa wa kwanza kulisabahi lango la wapinzani wao kupitia kwa David Ngog, lakini mshambuliaji wa Barmingham City Christian Benitez alifanikiwa kusawazisha bao hilo kwa mpira wa kichwa dakika chache baadae.
Bao la pili kwa upande wa Barmingham City lilipachikwa na mshambuliaji Cameron Jerome, kabla ya Gerrad kusawazisha kwa mkwaju wa penalti.
No comments:
Post a Comment