
Uongozi wa klabu ya Chelsea umerejesha dhamira yake ya kutaka kumsajili kiungo wa pembeni wa kimataifa toka nchini Ufaransa na klabu ya Bayern Munich Franck Ribery.
Chelsea wamerejesha dhamira hiyo baada ya kupewa nafasi ya kufanya usajili na mahakama ya michezo CAS ambayo imesogeza mbele adhabu yao ya kutosajili mchezaji yoyote kwa kipindi cha miaka mitatu iliyotolewa na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA.
Kufuatia kuwepo kwa dhamira hiyo uongozi wa klabu ya Chelsea umejipanga kumuhamisha Ribery mwezi januari mwakani katika dirisha dogo la usajili ambalo watalitumia kuziba mapengo yatakayoachwa na wachezaji wambao watajiunga na timu zao za taifa katika michuano ya kombe la Afrika.
No comments:
Post a Comment