Winga wa kimataifa toka nchini Ureno anayeichezea klabu ya Manchester United NANI amepinga mfumo unaotumiwa na meneja wake Sir Alex Ferguson kuwaongoza wachezaji wake.Winga huyo ambae anaonekana kushindwa kuziba pengo la anayeonakana Cristiano Ronaldo huenda akawa amajipalia makaa ya kuendelea kusalia Old Traford yalipo makao makuu ya klabu ya Man utd.
Akihojiwa na gazeti moja la huko nchini Ureno Nani amesema meneja huyo hajatimiza ahadi zake alizomuahidi ikiwa ni pamoja na kumuondoa kabisa katika kikosi cha kwanza hatua ambayo imepelekea kiwango chake kushuka siku hadi siku.
Nani amesema Ferguson ni mtu ambaye hatabiriki na asieleweka hivyo ana wakati mgumu kutumiza matarajio ya mashabiki wake kutokana na kutopata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu uwanjani na hivyo kushindwa kufunga mabao. 

Amesema mara nyingi akipata nafasi anacheza vizuri lakini amekuwa hana uhakika wa kupata nafasi katika mchezo ujao hali ambayo inamkatisha tamaa.
Amesema hakuota kuwa na bahati ya kucheza mechezo mikubwa dhidi ya klabu za Liverpool, Manchester City na Tottenham, mechi ambazo zinamjengea mchezaji uwezo ambapo mpaka sasa kwake binafsi ameshacheza michezo 13 na kufunga bao moja.
Akizungumzia tabia za meneja huyo Nani amesema Sir Alex Ferguson hana simile hasa pale anapoamua kumsema mchezaji mbele ya wachezaji wenzake tena kwa sauti bila hata kujali hata wachezaji wakongwe kama vile Ryan Giggs na Gary Neville ambao mara nyingi wamekuwa wakilaumiwa na kutukanwa.
Hatua hii ya Nani kumzungumzia meneja wake huenda ikahitimisha uwepo wake katika klabu hiyo hasa baadhi ya wachezaji waliwahi kudiriki kwenda kinyume na matakwa ya Ferguson ambao waliishia kuihama klabu hiyo.
Itakumbukwa kwamba beki wa kimataifa toka nchini Uholanzi aliyestaafu soka kwa sasa Jaap Stam aliwahi kuchapisha kitabu chake mwaka 2001 kilichukua kinazungumzia maisha yake ya soka na kumlaumu Ferguson ambaye aliamua kumuuza katika klabu ya Lazio kwa paundi milioni 16.5.Miaka miwili baadaye , David Beckham aliuzwa katika klabu ya Real Madrid baada ya kukorofishana na meneja huyo.
Mwezi Novemba mwaka 2005 ilikuwa ni zamu ya Roy Keane aliyejiunga na klabu ya Celtic kwa miezi sita ya maisha yake ya kucheza soka yaliyokuwa yamesalia baada ya kujibishana na meneja huyo kutokana na kutoridhidhwa na uwezo wa timu hiyo katika kipindi hicho.
Hatua hiyo ya Nani huenda ikahitimisha ndoto zake za kurithi nafasi ya Mreno mwenzake Ronaldo aliyehamia katika klabu ya Real Madrid miezi minne na nusu iliyopita baada ya kutumainiwa na wengi kwamba angeweza kuziba pengo hilo kutoka na kushabihana kiuchezaji.
Nani ambaye alisajiliwa na Ferguson kutoka klabu ya Sporting Lisbon mwezi July 2007 kwa ada ya paundi milioni 16 amesema pamoja na kuzungumza yote yaliyo moyoni mwake kuhusu Sir Alex Ferguson bado hana mpango wa kuihama klabu hiyo hivyo kinachosubiriwa ni hatua ambayo itachukuliwa na na babu.
No comments:
Post a Comment