





Majogoo wa jiji Liverpool usiku wa kumkia hii leo wamejikuta wakitupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya licha ya kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya klabu ya Debrecen.Liverpool wametupwa nje ya michuano hiyo kimahesabu kufuatia ushindi uliopatikana kwenye mchezo mwingine wa kundi la tano ambapo uliikutanisha timu ya Fiorentina dhidi ya Olympic Lyon.
Katika mchezo huo Fiorentina walifanikiwa kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri ambao unawawezesha kufikisha point 12 wakifuatiwa na Lyon wenye point 10 ili hali Liverpool wamesaliwa na point 7 ambazo haziwezi kuwapeleka popote hata wakishinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Fiorentina kwani watakuwa wamezidiwa idadi ya mabao ya kufungwa na kufunga.
Hata hivyo Liverpool watashiriki michuano ya ligi ya Ulaya baada ya kuangushwa kwenye michuano hiyo ya ligi ya mabingwa.
Michezo mingine iliyopigwa usiku wa kumakia leo ni pamoja na;
AZ Alkmaar 0-0 Olympiakos
Barcelona 2-0 Inter Milan
Fiorentina 1-0 Lyon
Rangers 0-2 VfB Stuttgart
Rubin Kazan 0-0 Dynamo Kiev
Unirea Urziceni 1-0 Sevilla
Barcelona 2-0 Inter Milan
Fiorentina 1-0 Lyon
Rangers 0-2 VfB Stuttgart
Rubin Kazan 0-0 Dynamo Kiev
Unirea Urziceni 1-0 Sevilla






Arsenal 2-0 Standard Liege
No comments:
Post a Comment