
Benchi la ufundi la klabu ya Sunderland limeingiwa hofu ya kumkosa mshambuliaji wao wa kimataifa toka nchini Uingereza Darren Bent ambae anadhaniwa huenda wakawa nje ya uwanja baada ya kuumia goti.
Mshambuliaji huyo aliumia goti baada ya kufunga bao la ushindi wa bao moja kwa sifuri uliopatikana mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya klabu ya Arsenal.
Meneja klabu hiyo maarufu kama Black Cats, Steve Bruce ameeleza katika mtandao wa klabu hiyo, kwamba iwapo vipimo vitaonyesha goti la mshambuliaji huyo limeumia kwa kiasi kikubwa, basi upo uwezekano mkubwa wa kumkosa kwa muda wa majuma matatu.
Kufuatia hofu hiyo Bent huenda asiwepo kwenye mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo Sunderland watakiputa na Wigan.
No comments:
Post a Comment