KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, December 11, 2009

CAMPBELL AISUBIRI SAFARI YA OLD TRAFFORD.


Beki wa zamani wa kimataifa toka nchini Uingereza Sol Campbell amesema angependa kujiunga na klabu ya Manchester United ili kuimarisha safu ya ulinzi ya klabu hiyo.

Sol Campbell ameyasema hayo baada ya meneja wa klabu hiyo Alex Ferguson kusema anafikiria kumsajili mchezaji huyo ambaye kwa sasa yu huru kusajiliwa na klabu yoyote .
Campbel mwenye umri wa miaka 35 amesema hawezi kusita kujiunga na mabingwa hao wa soka nchini Uingereza iwapo atahitajika.

Hata hivyo amesema kwa sasa hajapata taarifa yoyote kutoka kwenye uongozi wa mshetani hao wekundu na kama itatokea usajili wake utakuwa muhimu kwake.

Amesema kwa sasa anafanya mazoezi na klabu ya Arsenal na angependa kufanya mazoezi na Manchester United.

Campbell ameruhusiwa kucheza tena baada kumaliza sakata lake na klabu ya Notts County iliyokuwa imemsajili kwa mkataba wa miaka 5 lakini aliamua kuondoka baada ya kuichezea klabu hiyo mchezo mmoja.

Itakumbukwa kwamba meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger alimruhusu Campbell kufanya mazoezi na klabu hiyo ili kujiweka fit kabla ya kuruhusiwa kucheza tena na chama cha soka nchini Uingereza.

Kwa sasa safu ya ulinzi ya klabu ya Manchester United imekabiliwa na majeruhi wengi hali iliyomlazimu Ferguson kuwachezesha viungo wake Darren Fletcher na Michael Carrick katika safu hiyo kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi dhidi ya Wolfsburg ambapo katika mchezo huo Man Utd walishinda kwa mabao 3-1 .

No comments:

Post a Comment