KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, December 11, 2009

ANCELOTTI ABWATA


Inasemekana hivi karibuni meneja huyo alizungumza na wachezaji wake kwa muda wa dakika 15 baada ya kuonekana kutokufanya vizuri katika michezo ya hivi karibuni hasa baada ya kuruhusu kufungwa bao katika kipindi cha pili katika mchezo wa ligi ya mabingwa.

Akithibitisha hilo kiungo wa kimataifa toka nchini Nigeria John Obi Mikel amesema mazungumzo hayo yalikuwa machungu kwao tangu meneja hiyo alipoanza kuifundisha klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu.

Mikel amesema meneja wao alichukizwa na jinsi walivyocheza katika kipindi cha pili na kufikia hatua ya kuwapa mwanya wapinzani wao kusawazisha bao na kuufanya mchezo kumalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Ikumbukwe kuwa kiungo huyo wa kimataifa toka nchini Nigeria ni mmoja wa wachezaji ambao watakosekana kwenye kikosi cha Chelsea wakati michuano kombe la mataifa ya Afrika itakapoanza kutimia vumbi lake na Ancelotti anafikiria kumsajili kiungo wa zamani wa klabu ya Arsenal Patrick Vieira katika msimu wa dirisha dogo la usajili.

No comments:

Post a Comment