
Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amemelaumu meneja wa klabu ya Manchester United Alex Ferguson kwa kutomchezesha mshambuliaji Michael Owen kila mara.
Capello amesema anamfuatilia maendelea ya Owen lakini anashangazwa kutopewa nafasi na kujiuliza kwa nini meneja huyo anamchezesha Rooney kila mara.
Capello amesema Owen ni mchezaji muhimu na anadhani anastahili kupewa nafasi ili aweze kupata mwanya wa kucheza fainali za kombe la dunia.
Juma lililopia Owen mwenye umri wa miaka 30 alifunga mabao 3 katika mchezo wa ligi ya klabu bingwa barani ulaya dhidi ya klabu ya Wolfsburg lakini alijikuta akichezea dakika 15 katika mchezo wa ligi dhidi ya klabu ya Aston Villa mwishoni mwa juma lililopita.
No comments:
Post a Comment