Mshambuliaji huyo wa kimataifa toka nchini Bulgaria alijiunga na Manchester United kwa gharama ya paundi milioni 30.75 akitokea klabu ya Tottenham mwaka 2008 lakini ameshindwa kuzikonga baadhi ya nyoyo za mashabiki wa klabu hiyo.
Berbetov amesema kila mtu ana mbinu za kukabiliana na msongo wa mawazo na hivyo amekuwa na wakati mgumu wa kukabiliana na matarajio ya mashabiki wengi hasa wakizingatia gharama iliyotumika kumsajili akitokea Spurs.

Amesema pamoja na mashabiki wa klabu hiyo kumuona akifunga mabao, kutoa pasi na hata michezo aliyoichezea klabu hiyo, anajua bado wanahitaji afanye mengi kutokana na fedha zao walizotoa . Hata hivyo amewaahidi mashabiki hao kuwa atafanya kila jitihada ili aweze kuwalipa fadhila kwa uvumilivu wao kwake.
No comments:
Post a Comment