KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 16, 2009

EKOTTO KUMALIZA NA JAMAA YAKE!!


Mlinzi wa klabu ya Tottenham hotspurs Benoit Assou-Ekotto hatachunguzwa zaidi baada ya shabiki aliyegomban nae kufuta tuhuma za kushambuliwa na mchezaji huyo.

Assou-Ekotto, mwenye umri wa miaka 25, alihusika katika mzozo na shabiki mmoja wakati akitoka uwanjani mpira ulipomalizika baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Wolves siku ya Jumamosi.

Sasa Polisi hawataendelea tena na uchunguzi wao baada ya mchezaji huyo na shabiki kukubaliana kukutana wiki hii kumaliza mzozo wao kwa amani.

Kwa upande wao chama cha soka cha England nacho kimesema hakitachukua hatua zaidi kuhusiana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment