
Katika hatua nyingine Zikiwa zimesalia takriban wiki nne kabla kuanza mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Angola, wenyeji wanaendelea kukamilisha miundombinu yote.
Kazi za ujenzi zinaendelea katika viwanja, barabara na uwanja mkubwa wa ndege wa Luanda na hadi sasa tiketi hata moja haijauzwa .
nyasi z uwanja wa Luanda bado hazijafanyiwa taratibu zozote kutokana na mizozo ya mikataba.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa la AFP inavyoonekana hali itakuwa ni kukimbizana na wakati ili vitu viwe tayari kwa muda uliopangwa.
Lakini waziri wa ujenzi wa Angola Higinio Carneiro amesema hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi.
Amesema "viwanja vitakuwa tayari na hakutakuwa na tatizo lolote la kuandaa mashindano hayo itakapofika mwezi wa Januari."
No comments:
Post a Comment