
Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA imepanga kumchunguza ashambuliaji wa Ufaransa Thierry Henry kutokana na kitendo cha kuushika mpira katika mchezo wa mtoano wa kusaka nafasi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya Jamhuri ya Ireland.
Kufuatia kitendo hicho cha Henry ambacho kilisababishwa kupatikana kwa bao lililoizuia Jamhuri ya Ireland kufuzu kucheza fainali hizo.
Kamati kuu ya Fifa imekutana jana na kulijadiliana tukio hilo kama sehemu ya mambo ya kutupiwa macho ya nidhamu.
No comments:
Post a Comment