
Kocha wa Ghana Milovan Rajevac juma lijalo amepanga kukutana na mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan takutana na Mario Balotelli ili aweze kumshawishi kuichezea timu yake kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2010.
Balotelli mwenye umri wa miaka 19 anatarajiwa kukutana na ushawishi huo kufuatia kuwa na uraia wa nchini Italia lakini mpaka sasa ameshalichezea taifa katika timu ya taifa ya vijana michezo 21.
Balotelli mwenye asili ya nchini Ghana anakila sababu za kuicheza timu ya taifa ya Ghana kwenye fainali hizo kufuatia hatua ya kutokucheza katika timu kubwa ya taifa ya Italia.
No comments:
Post a Comment