KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 3, 2009

HUGHES AMSHANGAA WENGER.


Meneja wa klabu ya Man City, Mark Hughes, amemlaumu wazi wazi meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger kwa kitendo chake cha kukataa kumpa mkono mara baada ya mchezo wa hatua ya robo fainali baiona ya vikosi vyao vilipokutana usiku wa kuamkia leo huko City Of Manchester.

Hughes amesema Wenger hakustahili kuonyesha kitendo hicho kutokana na kila shabii wa soka ulimwnguni kumfahamu vyema tabia yake hivyo amejipunguzia heshima kwa kitendo chake cha kuondoka uwanjani bila kumpa mkono hatua mbayo huchukuliwa kama Fair Play.


Hughes ameongeza kwamba huenda wenger walichukizwa na kitendo cha kufungwa nah ii inatokana nay eye kuzoea kushinda kila anapopambana na timu pinzani.


Hata hivyo kauli hiyo ya Mark Hughes imejibiwa na meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ambapo amesema anadhani yeye ni mtu mwenye akili na hawezi kuchaguliwa ni yupi ampatie mkono wake mara baada ya kikosi chake kumaliza hatua ya kushindana.

1 comment:

  1. Wenger ni mshamba na ndio maana alikua hapatani na kocha wazamani wa Chersea Jose morinyo,kwani Wenger ni mtu anayejiona kuwa mbabe na mwenye uwezo mkubwa sana zaidi ya mtu mwingine,kipindi hivi sasa hata historia nzuri aliyokuwa nayo imeanza kutoweka kwa jinsi anavyopigwa kila kukicha.Yani ile ya kupeana mkono kwa makocha wakimaliza mchezo, inaotufunza mambo mengi ya undugu ndani ya michezo.Kwanza Weger angestahili kupewa adhabu hata ndogo.

    ReplyDelete