KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 3, 2009

FIFA NA MAANDALIZI YA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA.



Fifa imekataa mipango ya kuanza kuwatumia waamuzi wa ziada katika mashindano yajayo ya Kombe la Dunia ya mwaka 2010.

Shirikisho hilo la soka ulimwenguni kote lilikuwa likijadili suala hilo baada ya utata wa bao la Ufaransa ambapo Thierry Henry aliushika mpira katika mchakato wa kumpelekea mpira mfungaji.

Henry aliushika mpira mara mbili kabla bao lililoipatia nafasi ya kufuzu Ufaransa walipocheza na Jamhuri ya Ireland .

Lakini Rais wa Fifa Sepp Blatter ameeleza uchunguzi utaendelea kwa ajili ya kutathmini manufaa ya kutumia teknolojia ya video na waamuzi wa ziada.

No comments:

Post a Comment