
Meneja wa klabu ya Fulham Roy Hodgson amesema ana imani beki wake wa kulia toka nchini Ghana John Pantsil atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaoisaidia klabu yake kwenye mchezo wa Disemba 28 dhidi ya Chelsea.
Hodgson ametoa kauli hiyo kufuati amvutano uliopo baina ya klabu ya Fulham dhidi ya chama cha soka nchini Ghana ambacho kinamtaka mchezaji huyo ili aweze kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Disemba 27 kwa ajili ya maandalizi ya fainali za mataifa ya Afrika.
Katika mvutano huo chama cha soka nchini Ghana kimeshatoa kauli yake ya kuhakikisha beki huyo anaruhusiwa kwa muda muafaka ili aweze kutimiza sharti la kujiunga na wenzake kambini.
Hata hivyo meneja wa klabu ya Fulham ameshatoa taarifa inayoeleza kwamba iwapo shisrikisho la soka ulimwenguni kote hawatoingilia kati mvutano huo watamtumia Pantsil Disemba 28 na endapo shisrikisho hilo likiingilia kati atakuwa mpole na kumruhusu aondoke.
Sheria za Fifa zinasema vilabu havina budi kuwaachilia wachezaji wao siku 14 kabla ya kuanza mashindano ya kimataifa yanayotambuliwa ulimwengini kote.
Endaopo FIFA wataingili akati na kubaini Fulham watafanya makosa itawapokonya point ambazo watazipata katika mchezo huo na Chelsea iwapo Pantsil atacheza pambano hilo.
Mchezaji mwengine ambaye yupo katika mzozo baina ya klabu na nchi ni Madjid Bougherra kutoka Algeria.
Klabu yake ya Rangers inajaribu kuiomba Algeria imruhusu kucheza mechi dhidi ya Celtic Januari 3 mwakani.
No comments:
Post a Comment