KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, December 14, 2009

WAGONGA NYUNDO WAMUAWANI ADRIANO.


Wagonga nyundo wa jijini London West Ham Utd wana matarajio makubwa uya kumsajili mshamuliaji wa zamani wa klabu ya Inter Milan ya nchini Italia Adriano ambae kwa sasa anaitumikia klabu ya Flamingo ya nchini kwao Brazil.

West Ham Utd wameweka matarajio hayo kwa lengo la kutaka kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji wao Dean Ashton ambae ametangaza kustahafu soka kufuatia jeraha lake la mguu kutoonyesha dalili za kupona kabisa.

Meneja wa klabu ya West Ham Utd Gianfranco Zola kwa sasa anaonekana kutaka kutengeza safu imara ya ushambuliaji na endapo atampata mshambuliaji huyo uwezekano huo huenda ukafanikiwa kufuatia kwa sasa kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa kama David di Michele pamoja na Diego Tristan.

No comments:

Post a Comment