
Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Stoke James Beattie anafikiria kuondoka katika klabu hiyo kufuatia mzozo na meneja wake Tony Pulis.
Pulis na Beattie iliwabidi watenganishwe katika chumba cha kuvalia baada ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Arsenal.
Hata hivyo jana uongozi wa klabu ya Stoke ulitoa taarifa za kufanya uchunguzi kufuatia taarifa za mzozo huo ambapo hadi sasa Beattie hajamuomba msamaha Pulis.
Beattie mwenye umri wa miaka 31 amebakiwa na miezi 18 kabla ya kumaliza mkataba wake akiwa amejiunga na klabu hiyo mwezi wa Januari mwaka huu.
Amekuwa mchezaji wa kutumainiwa katika klabu hiyo wakati mabao yake saba wakati wa msimu uliomalizika yaliisaidia klabu hiyo kuendelea kusalia katika Ligi Kuu ya soka ya England.
No comments:
Post a Comment