
Beki wa klabu ya soka ya Ligi Kuu ya England Portsmouth Linvoy Primus ametangaza kustaafu kucheza soka baada ya goti lake kuonekana kutopona kabisa.
Primus mwenye umri wa miaka 36 hajacheza mchezo wowote msimu huu na madaktari wamemshauri asicheze tena soka baada ya kufanyiwa upasuaji zaidi wa goti.
Awali matatizo ya goti yalimfanya kutocheza mwaka 2007, Primus kwa sasa atafanya kazi ya ubalozi kwa klabu yake ya Portsmouth.
Amesema ni bora zaidi kuwa na goti zima kwa maisha yake yote kuliko kujaribu kucheza soka na kuliharibu kabisa.
Primus, alijiunga na klabu hiyo kwa uhamisho huru akitokea klabu ya Reading mwaka 2000, na alisaini mkataba wa mwaka mmoja tu na Portsmouth mwezi Julai mwaka huu.
No comments:
Post a Comment