
Uongozi wa klabu ya Stoke City umetangaza kufanya uchunguzi wa chanzo cha mtafaruku ambao ulipelekea ugomvi kati ya mshambuliaji wa klabu hiyo James Beattie dhidi ya meneja Tony Pulis baada ya mchezo wa ligi kuu mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Arsenal.
Taarifa zimeeleza kuwa kufuatia ugomvi huo ililazimika kuchukuliwa hatua ya kuwatenganisha wagomvi hao vyumba baada ya kulumbana na kushikana mashati walipokuwa katika chumba cha kubadilishia.
Hata hivyto imeelezwa kuwa bado kulionekana kuwepo kwa hali ya kutoelewana kati ya wagomvi hao na kufikia hatua ya Beattie kutokufanya mazoezi na wenzake ingawa alifika uwanjani na kuondoka baada ya nusu saa.
No comments:
Post a Comment