KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, December 8, 2009

MESSI NDANI YA BAHATI NYINGINE.


Kiungo mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo nyingine msimu huu baada ya kutwaa tuzo ya mchezji bora wa barani Ulaya juma lililopita.

Tuzo hiyo ambayo Messi anapigiwa upatu aipate ni tuzo ya mchezaji bora wa dunia ambayo anawani na wachezaji wenzake toka katika klabu ya Barcelona ambao ni Andres Iniesta pamoja na Xavi Harnandes huku klabu ya Real Madrid ikiwatoa wachezaji wawili katika kinyang’anyiro hicho ambao ni Kaka pamoja na Cristiano Ronaldo.

Hafla ya kutangazwa kwa mshindi wa tuzo hiyo inatarajiwa kufanyika mjini Zurich nchini Uswiz mnamo December 21.


kwa upande wa wanawake wanaowania tuzo kama hiyo kwa mwaka huu ni;


Cristiane (Brazil)


Inka Grings (Germany)


Marta (Brazil)


Birgit Prinz (Germany)


Kelly Smith (England)

No comments:

Post a Comment