KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 10, 2009

SUNDERLAND KIMEO?


Meneja wa klabu ya Sunderland Steve Bruce anaendelea kupata mitihani katika kikosi chake baada ya kuthibitishiwa na jopo la madaktari wa klabu hiyo kwamba beki wake Anton Ferdinand huenda akawa nje ya uwanja kwa muda wa majuma manne yajayo.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 24 amepata mkasa wa kuwa nje ya uwanja kufuatia kugongana na mshambuliaji wa klabu ya Fulham Erik Nevland mwishoni mwa juma lililopita ambapo mchezo huo ulishuhudia The Cottegers wakichomoka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Meneja wa klabu ya Sunderland Steve Bruce amekiambia moja ya chombo cha habari nchini Uingereza kwamba beki huyo amepata maumivu ya kifundo cha mguu wakati akianguka chini mara baada ya kugongana na Erik Nevland.

No comments:

Post a Comment