
Klabu ya Chelsea huenda ikamkosa kiungo wake Michael Essien kwa muda wa miezi miwili kufuatia kuumia kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya klabu ya APOEL Nicosia.
Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa Essien ameumia na anaweza kukaa nje ya dimba kwa muda wa majuma manne.
Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa Essien ameumia na anaweza kukaa nje ya dimba kwa muda wa majuma manne.
Iwapo hali itakuwa hivyo nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ghana atatakiwa kurejea uwanjani wakati muafaka na ataweza kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Africa mwezi January mwakani.
Kuumia kwa Essien ni pigo kubwa kwa meneja wake Carlo Ancelotti ambaye hadi sasa amepoteza michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja sambamba na kupoteza mchezo mmoja katika michezo mitatu iliyopita.
No comments:
Post a Comment