KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, December 18, 2009

TRAORE APEWA SHAVU.


Shirikisho la Soka nchini Senegal (FSF) limemteua Amara Traore kuwa kocha mpya wa timu ya taifa inayojulikana kama Teranga Lions.

Traore mwenye umri wa miaka 44 ameteuliwa kushikwa wadhifa huo baada ya kuifundisha klabu ya daraja la kwanza ya ASC Linguere de St-Louis tangu mwaka 2007, ambapo ameshaiwezesha kutwaa ubingwa msimu huu.

Tangu mwezi Oktoba mwaka 2008 timu ya taifa ya Senegal imekuwa haina kocha kufuatia ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Lamine Ndiaye kufuzwa kazi kutokana na kushindwa kuiwezesha timu hiyo kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2010.


Jukumu la kwanza Traore alilopewa ni kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa barani Afrika 2012 na michezo ya Olimpiki.

2 comments:

  1. Ndugu yangu
    Kwa niaba ya familia yangu na wapenda mema wote nakutakia kila lililo jema wakati huu wa sikukuu na usalama kuelekea mwaka mpya
    Baraka kwako

    ReplyDelete
  2. Mzee umepotelea wapi?mbona siku za mapumziko zimeisha?yanii blog imesinzia kabisaa,,,kaza misuli mzee tuendeshe hili libeneke.

    ReplyDelete