
Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Michael Owen sasa atakua nje ya uwanja kwa muda wa kipindi cha msimu kilichosalia.
Taarifa za mshambuliaji huyo zimetolewa uthibitisho huo hii leo, baada ya kufanyiwa uchunguzi, kufuatia kuumia kwenye mchezo wa hatua ya faianali ya kombe la ligi ulioshuhudia Man utd wakiibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Aston Villa.
Taarifa hizo zimeeleza kwamba Owen ameumia nyonga na huenda hali hiyo ikampelekea kuzikosa fainali za kombe la dunia zitakazounguruma nchini Afrika kusini kuanzi June 11 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment