KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, March 17, 2010

SAFARI YA CHELSEA YAFIKIA UKINGONI


Mabingwa wa soka nchini Italia Inter Milan wamefuta mipango na ndoto na matajiri wa London Chelsea ya kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kufuatia kipondo cha bao moja kwa sifuri walichokitoa usiku wa kuamkia leo huko Stamfod Bridge.

Chelsea walijikuta wakipotezewa mipango na ndoto zao kufuatia bao lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Cameroon Samuel Eto’o dakika 15 kabla ya pambano hilo kumalizika.

Kwa ushindi huo Chelsea wamesukumwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa idadi ya mabao matatu kwa moja.


Mchezo mwingine wa ligi ya mabingwa uliochezwa jana ulikua kati ya Sevilla ya Hispania dhidi ya CSKA MOSCOW ambapo mchezo huo ulimalizika kwa kushuhudia warusi wakisonga mbele kufuatia kup[ata ushindi wa mabao mawili kwa moja.

No comments:

Post a Comment