KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, March 15, 2010

BECKHAM KWENYE HATI HATI


Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza David Beckham huenda akazikosa fainali za kombe la dunia kufuatia maumivu aliyoyapata kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Italia hapo jana dhidi ya wakombozi wang’ambo Chievo Verona.



Maumivu hayo ambayo yanahofiwa kuwa chanzo cha Beckham kuzikosa fainali hizo, yanatokana na kushtua kifundo cha mguu wake wa kushoto alipokua kwenye harakati za kutaka kutoa pasi kwa mchezaji mwenzake.



Kiungo huyo mwenye umri mwenye umri wa miaka 34 alilazimika kutolewa uwanjani huku akiwachia simanzi mashabiki wake waliokua wakimtarajia kuonekana akiwa na timu yake ya taifa ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment