Beki wa klabu ya Arsenal William Gallas amefanikiwa kupiga mpira kwa mara ya kwanza toka alipoumia kweye mchezo wa hatua ya robo fainali kati ya klabu yake dhidi Barcelona.
Hatua ya beki huyo kupiga mpira kwa mara ya kwanza toka mwezi March inatoa nafasi kwa mashabiki wa soka huko Ufaransa kutarajia kumuona Gallas kwenye fainali za kombe la dunia zitakazoanza majuma matatu yajayo nchini Afrika kusini.
Pamoja na Gallas mwenye umri wa miaka 32 kuonyesha hali ya kutokupona kwa wakati siku kadhaa zilizopita, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Raymond Domenech alionesha kumuamini na kumthamini baada ya kumjumuisha kwenye kikosi chake kinachotarajia kucheza fainali za kombe la dunia.

No comments:
Post a Comment