Meneja wa kimataifa toka nchini Israel Avram Grant ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya kuinoa klabu ya Portsmouth iliyoshuka daraja kwenye ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu wa mwaka 2009-10.
Grant ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo huku akiwaacha njia panda mashabiki wa klabu ya Portsmouth ambao wanajiuliza ni wapi muyahudi huyo atakapoelekea.
Hata hivyo taarifa za fununu tayari zimeshaeleza kwamba Grant ameahidiwa donge nono huko Upton Park yalipo makao makuu ya klabu ya West Ham Utd.
West Ham Utd wapo mbioni kumchukua meneja huyo baada ya kumtimua aliekua meneja wao Gianfranco Zola mara baada ya msimu wa mwaka 2009-10 kumalizika.

No comments:
Post a Comment