KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Ureno, Carlos Queiroz amesema kikosi chake kitacheza fainali za Kombe la Dunia kikiwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi wa taji hilo.
Kocha huyo msaidizi wa zamani wa timu ya Manchester United, jana alisema kuwa, kama siyo kutwaa ubingwa timu yake itakuwa miongoni mwa timu nne zitakazofika hatua ya mwisho katika fainali hizo zitakazofanyika kunzia Juni 11 hadi Julai 11 mwaka huu nchini Afrika Kusini.
"Ureno ni moja ya timu zenye nafasi katika mbio za kuwania nafasi hiyo," alisema kocha Queiroz. " Historia katika Kombe la Dunia inaonesha mara zote tunakuwa kati ya timu tatu zinazofika nusu fainali, hivyo Ureno na timu nyingine 15 ndizo zitakazokuwa zikiwania nafasi hiyo," aliongeza kocha huyo.
Kwa mujibu wa kocha huyo mzaliwa wa Msumbiji, timu watakazokuwa wakichuana nazo ni Brazil, Italia, England, Ujerumani, Hispania na Argentina.
"Kila mechi tuna nafasi ya kushinda. Tunalifahamu hilo na jambo kubwa la msingi wapinzani wetu wanalifahamu jambo hilo vyema," alisema Queiroz ambaye kwa mara ya kwanza katika historia kikosi chake kilitinga nafasi ya tatu katika viwango vya FIFA.
Alisema kuwa, ana matumaini wakati watakapokutana na Brazili katika mechi ya tatu, watakuwa tayari wamefuzu na akasema kuwa, lakini mahesabu yao yatakuwa ni kutoonesha masihara kwa wapinzani wao wengine wawili.
Ureno imewahi kutinga nusu fainali katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2006 na 1966, katika fainali za mwaka huu imepangwa kundi G ambalo linasemekana kuwa, kundi la kifo ikiwa na timu za

No comments:
Post a Comment