KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Sunday, May 23, 2010

Rais Jonathan aitaka Nigeria kurudi na kombe.


RAIS wa Nigeria, Goodluck Jonathan ameitaka timu ya taifa ya nchi hiyo 'Super Eagles' kurejea nyumbani na tuzo kubwa katika medani ya soka wakati ikitokea nchini Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.

Rais Jonathan ambaye mwishoni mwa wiki alisema kuwa, atahudhuria sherehe za ufunguzi zitakazofanyika Juni 11, mwaka huu wakati Afrika Kusini itakapokuwa ikiumana na Mexico, alisema ataishuhudia mechi ya kwanza kati ya Nigeria na Argentina itakayopigwa Juni 12 kwenye Uwanja wa Ellis Park uliopo mjini Johannesburg.

Katika fainali hizo, Nigeria imepangwa kundi B ikiwa na timu za Argentina, Korea Kusini na Ugiriki na rais huyo anatarajia kuona timu hiyo ikisonga hatua ya pili na hatimaye fainali.

Akizungumza wakati wa chakula maalum cha kuiaga Super Eagles kwenda kwenye fainali hizo Ijumaa, Rais Jonathan alizungumzia pia maadhamisho ya siku ya kutimiza miaka 50 ya Uhuru wa nchi hiyo yatakayofanyika Oktoba mosi akisema kuwa, jukumu hilo ni la kitaifa na akasema anatarajia Super Eagle itajiandaa vyema na kushinda taji hilo ambalo ltakuwa ni zawadi kwa maadhimisho hayo.

Timu hiyo iliondoka Jumamosi asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Nnamdi Azikiwe uliopo mjini Abuja kwenda London kwa ajili ya kujiandaa na fainali hizo.

Mfanikio makubwa ambayo iliyapata Nigeria katika fainali za Kombe la Dunia ilikuwa ni mwaka 1994 na 1998 ambako timu hiyo ilifika hatua ya pili.

No comments:

Post a Comment