KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 25, 2010

MBADALA WA BLANC APATIKANA.


Baada ya kufahamika Laurent Blanc atajiunga na timu ya taifa ya Ufaransa mara itakaporejea kutoka kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka huu uongozi wa klabu ya Bordeaux umemtangaza Jean Tigana kuwa meneja mpya wa klabu hiyo.

Maamuzi ya uongozi ya klabu hiyo yamefikiwa kufuatia Laurent Blanc kupewa mkono wa kwa heri kati kati ya juma lililopita baada ya mazungumzo dhidi ya viongozi wa shirikisho la soka nchini Ufaransa kukamilika.
Raisi wa klabu ya Bordeaux Jean-Louis Triaud hii leo amemtambulisha Jean Tigana, mbele ya waandihsi wa habari huku akibainisha wazi kuwa wana imani na meneja huyo juu ya kusaka mafanikio zaidi katika michuano mbali mbali watakayoshiriki msimu ujao.

Jean Tigana mwenye umri wa miaka 54 bado anakumbukwa kwenye medani ya soka kufuatia mipango yake aliyoiweka alipokinoa kikosi cha klabu ya Olympic Lyon na Monaco zote za Ufaransa pamoja na klabu ya Fulham ya nchini Uiungereza.

No comments:

Post a Comment