
Cesc Fabregas ametaka maombi ya mwanae ya kutaka kuihama klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Barcelona yafanyiwe kazi haraka iwezekanavyo.
Baba wa kiungo huyo ametoa msisitizo huo alipohojiwa na kituo kimoja cha radio mjini Barcelona ambapo amesema tayari mwanae ameshaonyesha nia ya kutaka kurejea nyumbani hivyo haoni sababu za ombi lake kucheleweshwa.
Amesema makubalia kati ya uongozi wa klabu ya Arsenal pamoja na ule wa klabu ya Barcelona hayapaswi kuchukua muda mrefu kama ilivyo sasa kwani anaamini endapo watafuata ombi la muhusika mazungumzo hayo yatachukua muda mfupi.
Hata hivyo taarifa zilizopatikana usiku wa kuamkia hii leo zimeeleza kuwa uongozi wa klabu ya Arsenal umeutaka uongozi wa klabu ya Barcelona kulipa kiasi cha paund million 80 kama ada ya uhamisho wa kiungo huyo.
No comments:
Post a Comment