KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 25, 2010

MOURINHO AANZA MAKEKE.


Baada ya kubainika huenda akajiunga na klabu ya Real Madrid msimu ujao, vyombo vya habari barani ulaya vimeanza kumfuatilia meneja wa klabu ya Inter Milan Jose Mourinho.


Moja ya ufuatiliji huo ni mipango ya usajili ambayo huenda ikafanywa na meneja huyo wa kimataifa toka nchini Ureno ambae amepewa kipaumbele cha kupelekea mabadiliko huko St Bernabeu.


Vyombo hivyo vya habari vimeripoti kuwa Jose Mourinho huenda akawasajili baadi ya wachezaji aliokua nao kwenye klabu ya Chelsea pamoja na Liverpool zote za Uingereza.


Miongoni mwa wachezaji hao lipo jina la mshasmbuliaji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast Didier Drogba, kiungo wa kimataifa toka nchini Ghana, Michael Essien, kipa wa kimataifa toka jamuhuri ya Czech Petr Cech , Lampard pamoja na Ashley Cole wote kutoka nchini Uingereza.

Mbali na wachezaji hao pia Mourinho anasemekana huenda akawasajili wachezaji wawili kutoka kwenye klabu ya Liverpool ambao ni nahodha wa klabu hiyo Steven Gerrard pamoja na mshambuliaji Fernando Torres.


Vyombo hivyo vya habari vimeendelea kubainisha kuwa Mourinho amepata jeuri ya kutarajia kuwasajili wachezaji hao kufuatia ahadi ya fedha alizo ahidiwa na viongozi wake watarajiwa toka Real Madrid.

No comments:

Post a Comment