KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Sunday, May 23, 2010

Montolivo: Ndoto yangu ni fainali Kombe la Dunia.


KIUNGO wa Fiorentina, Riccardo Montolivo ana matumaini ya kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha timu ya Taifa ya Italia kinachonolewa na kocha Marcello Lippi kinachojiandaa na fainali za Kombe la Dunia.

Mchezaji huyo kwa sasa ni kati ya wachezaji walioitwa katika kikosi cha awali, lakini ataifahamu hatma yake Juni mosi wakati kocha huyo atakapotangaza wachezaji 23.

Mchezaji huyo alisema kuwa, ana matumaini na kuanzia sasa ataonesha cheche zake katika kikosi hicho cha la Nazionale mpaka atakapopata nafasi ya kwenda Afrika Kusini.

"Matumaini yangu makubwa ni kwenda Afrika Kusini, kucheza kwenye fainali za Kombe Dunia, ndiyo ndoto yangu kubwa," kiungo huyo aliiambia tovuti ya klabu ya Fiorentina.

"Nina furaha katika mwaka huu na nina matumaini nitakwenda. Tangu nikiwa mtoto mawazo yangu yote yalikuwa ni kuichezea timu ya Taifa na yatakuwa maajabu makubwa kwangu," alisema.

No comments:

Post a Comment