
Siku kadhaa baada ya kumuachia mshambuliaji wao wa kimataifa toka nchini Hispania, David Villa aliejiunga na klabu ya Barcelona mwanzoni mwa mwezi huu, uongozi wa klabu ya Valencia umethibitisha kuendelea kuwauza nyota wake baada ya kukubali kufanya mazungumzo na klabu ya Man City juu ya kumuuza kiungo David Silva.
Raisi wa klabu ya Valencia Manuel Llorente hii leo amejitokeza kwenye umma wa waandishi wa habari na kubainisha wazi kwamba mwanzoni mwa juma lijalo uongozi wa klabu ya Man city utaanza mazungumzo dhidi yao ya kumsajili Silva.
Hata hivyo Manuel Llorente amebinisha kuwa kiungo huyo tayari walikua wameshamuweka sokoni, na klabu za Manchester United, Real Madrid pamoja na Barcelona zilionyesha nia ya kutaka kumsajili lakini Manchester City wamekua ya kwanza kutuma ofa.
David Silva mwenye umri wa miaka 24, anakadiriwa huenda akauzwa huko city of Manchester kwa kiasi cha paund million 30.
Uongozi wa klabu ya Valencia umeingia kwenye harakati za kuwauza nyota wake kutokana na deni kubwa linalowakabili ambapo siku mbili zilizopita uongozi huo ulikamilisha utaratibu za kumuhamisha Nikola Zigic kwenye klabu ya Birmingham city ya nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment