Baada ya kumuachia Jose Mourinho, uongozi wa klabu ya Inter Milan upo mbioni kumshawishi kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello ili aweze kuchukua pahala palipoacha wazi wa mreno huyo.
Akizungumza kwa niaba ya uongozi, raisi wa klabu ya Inter Milan Massimo Moratti amesema mbali na kocha huyo wa timu taifa ya Uingereza pia wapo makocha wengine ambao wanadhani huenda watafaa kuchukua nafasi ya kuwa meneja wa kikosi chao.
Amesema katika orodha hiyo jina la Capello linapewa nafasi kubwa kufuatia kuwa na sifa ya kuhimili mikiki mikiki ya ligi kuu ya soka nchini Italia pamoja na ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Moratti ameongeza kuwa kwa sasa wanahitaji kuwa na meneja ambae ataendeleza mazuri yalyoachwa na Jose Mourinho ambae mwishoni mwa juma lililopita aliwazadia ubingwa wa Ulaya.
Itakumbukwa kuwa Fabio Capello kabla hajasaini mkataba wa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, alikuwa meneja wa klabu ya Real Madrid ambayo aliizawadia ubingwa wa Hispania msimu wa mwaka 2007–08.
Capello pia ana hitoria ya kuzifundisha klabu ya Juventus, AC Milan pamoja na AS Roma.

No comments:
Post a Comment