KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 3, 2010

ARSENAL WAKATAA KUMTOA FAB.


Uongozi wa klabu ya Arsenal umekataa ofa ya klabu ya Barcelona iliyotumwa klabuni hapo jana mishale ya jioni kwa lengo la kumsajili nahodha na kiungo Francis Cesc Fabregas.

Taarifa zilizotolewa na uongozi wa klabu hiyo ya jijini London zimeeleza wazi kwamba kiungo huyo hauzwi huku uongozi wa klabu ya Barcelona ukitakiwa kuheshimu maamuzi yaliyotolewa.

Aidha Arsenal wameeleza wazi kwamba Fabregas bado ana mkataba wa miaka minne hivyo halitokua jambo la burasa kuusitisha mkataba huo na kuanza kuzungumza biashara ya kumuuza.

Itakumbukwa kuwa Fabreagas alisaini mkataba wa miaka minane mwaka 2006 na utaratibu huo unaendelea kumfanya kuwa mchezaji halali wa klabu ya Arsenal mpaka mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment