Winga wa kimataifa toka nchini Ureno Luis Boa Morte amepewa mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia wagonga nyundo wa London West Ham Utd.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 32, amepewa mkataba huo huku akiwa na kumbu kumbu ya kurejea uwanjani mwezi April mwaka huu baada ya kuwa nje ya uwanja alipokua akiuguza jeraha la goti lake ambalo lilidhaniwa huenda lingekua sababu za kuamuriwa aondoke katika kipindi hiki ha usajili.
Wakati winga huyo akikabidhiwa mkataba mpya, uongozi wa klabu ya West utd umetangaza kuwatema washambuliaji wake wawili waliosajiliwa klabuni hapo mwanzoni mwa mwaka huu kupitia dirisha dogo la usajili.
Washambuliaji wao ni pamoja na Mbrazil Ilan mwenye umri wa miaka 29 sambamba na Ahmed Hossan Mido toka nchini Misri mwenye umri wa miaka 27.
Sababu za kuachwa kwa washambuliaji hao hazijaelezwa wazi, lakini fununu zaeleza kwamba huenda viwango vya uchezaji wao hakijawaridhisha viongozi wa ngazi za juu wa klabu ya West Ham Utd.

No comments:
Post a Comment