KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, June 5, 2010

HIDINK AIKANA KAZI.


Kocha mpya wa timu ya taifa ya Uturuki Guus Hiddink amesema hana mpango wowote wa kujiunga na klabu ya Liverpool iliyo kwenye harakati za kusaka meneja mwingine baada ya kuondoka kwa Rafael Benitez siku mbili zilizopita.

Taarifa zilizotolewa na wakala wa kocha huyo Cees van Newhuzn zimeeleeza kuwa Hidink ameshtushwa na taarifa zinazomuhusisha kujiunga na klabu hiyo ya nchini Uingereza.

Wakala huyo amesema mteja wake kwa sasa anafikiria namna ya kuisaidia timu ya Uturuki kufuzu kucheza fainali za kombe la ulaya mwaka 2012 baada ya kushindwa kufuzu kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka huu.

Amesema kufuatia fikra hizo, Hidink bado anauheshimu mkataba wake aliosaini na viongozi wa shirikisho la soka nchini Uturuki.

Hata hivyo wakala huyo ameongeza kwamba tayari Hidink ameshaikataa ofa ya kujiunga na klabu ya Inter Milan ambayo nayo inamsaka mrithi wa Jose Mourinho alietimkia Real Madrid.

Mbali na Hidink, majina ya mameneja wengine wanaotajwa kuchukua nafasi ya Benitez huko Anfiled ni pamoja na meneja wa klabu ya Fulham Roy Hodgson, Louis van Gaal anaekinoa kikosi cha Bayern Munich, Martin O’Neill wa klabu ya Aston Villa, aliekua meneja wa klabu ya Manchester City Mark Hughes, Frank Rijkaard (Galatasaray S.K.) pamoja na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Croatia Slaven Bilic.

No comments:

Post a Comment