KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 4, 2010

FERDNAND NAE MASHAKANI WORLD CUP 2010.


Beki na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Rio Ferdinand nae hii leo alilazimika kukimbizwa hospitalini kufuatia kuumia goti katika dakika za mwishoni za mazoezi ya timu hiyo iliyowasili barani Afrika hapo jana.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 31 alipatwa na maswahiba hayo alipokua kwenye harakati za kuondoa hatari katika upande wa lango lake.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya uingereza Fabio Capello alizungumzia suala hilo kwenye mkutano na waandishi wa habari huku akibainisha wazi kwamba ana imani beki huo atapona kwa wakati na kuuwahi mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Marekani mnamo June 12.

Katika hatua nyingine Capello amesema mbali na beki huyo pia kipa David James hii leo hakufanya mazoezi kufuatia maumivu ya goti yanayomsumbua toka walipowasili jana huku sababu ikitajwa kuwa safari ndefu toka Uingereza mpaka Afrika kusini.

Pia Capello amethibisha taarifa za kuanza mazoezi kwa kiungo wa klabu ya Man City Gareth Barry aliekua anasumbuliwa na maumivu ya goti toka May 5 tano mwaka huu mara baada ya mchezo wa klabu yake dhidi ya Tottenham Hotspours.

No comments:

Post a Comment