KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 9, 2010

NI HESHIMA KWA WAAFRIKA !!!!


Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto'o amesema anaamini michuano ya fainali za kombe la dunia za mwaka huu huenda zikachochea kwa kiasi kikubwa kupunguza tabaka la ubaguzi wa rangi.

Samuel Eto'o amelizungumza suala hilo huku yeye akiwa ni mmoja wa wachezaji soka ambao mara kadhaa wamekua wakikumbwa na tabaka la ubaguzi wa rangi wanapokua kwenye vilabu vyao barani Ulaya.

Amesema bara la Afrika kupewa heshima ya kuandaa fainali za kombe la dunia ni dalili tosha za kuashiria ulimwengu mzima ni kitu kimoja hivyo itawafanya wabaguzi wa rangi toka katika mataifa mbali mbali kutambua hakuna tofauti ya binaadamu katika huu ulimwengu.

Mbali na suala hilo Eto’o ameongeza kuwa, suala la ubaguzi wa rangi pia litakoma, na bara la Afrika kuheshimika, kama mabara mengine, endapo moja ya timu inayoliwakilisha bara hilo katika fainali za kombe la dunia itatwaa ubingwa katika ardhi ya nyumbani.

No comments:

Post a Comment