KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 9, 2010

NANI NJE KOMBE LA DUNIA.


Winga wa klabu ya Man Utd Louis Nani ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakao zikosa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 zitakazoanza kutimau vumbi lake mwishoni mwa juma hili huko nchini Afrika kuisni.

Nani ameingia karika orodha ya wachezaji watakaozikosa fainali hizo, baada ya kuumia bega lake la kushoto alipokua kwenye maandalizi ya ya timu ya taifa ya Ureno ambayo iliweka kambi mjini Lisbon.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 23, imeelezwa kuwa aliumia bega siku ya ijumaa ya juma lililopita ikiwa ni muda mchache kabla ya Ureno hawajasafiri kuelekea nchini Afrika kusini.

Hata hivyo tayari nafasi ya Nani aliepachika mabao 11 kwenye harakati za timu ya taifa ya Ureno ilipokua ikisaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia imechukuliwa na kiungo wa klabu ya Benfica Ruben Amorim.

Amorim ameitwa kwenye kikosi cha Ureno huku akikumbukwa na mashabiki wengi wa nchi hiyo katika harakati zake za kuisaidia klabu yake ya Benfica kutwaa ubingwa wa Ureno kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano.


No comments:

Post a Comment