KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, June 5, 2010

ROBEN MASHAKANI !!!!!!!!!!!

Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Bayern Munich Arjen Robben atalazimika kusubiri vipimo ambayo vitamuamuru kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi watakaocheza kwenye fainali za kombe la dunia.

Roben ameingia katika wimbi la sintofahamu kufuatia kuumia nyonga kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Hungary iliyokubali kisago cha mabao sita kwa moja.

Katika mchezo huyo Robben alichukua nafasi ya mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Dirk Kuyt, kipindi cha pili na alipatwa na maswahiba ya maumivu ya nyonga katika dakika ya 85 baada ya kupachika mabao mawili katika dakika ya 64 na 78.

Mabao mengine ya Uholanzi katika mchezo huo yalikwamishwa wavumi na Robin van Persie, Mark van Bommel pamoja na Elia.

No comments:

Post a Comment