

Beki wa klabu ya Tottenham Hotspours Michael Dawson amefanikiwa kuwasili kwa wakati nchini Afrika kusini na kuanza mazoezi na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Uingereza.Michael Dawson ameanza mazoezi na kikosi cha Capello mara baada ya kutajwa kama mbadala wa Rio Ferdinand ambae kwa sasa anauguza jeraha la goti alilolipata jana akiwa mazoezi.
Beki huyo mwenye umri wa 26, imemchukua muda wa saa 24 kusafiri toka nchini Uingereza, kufuatia taarifa iliyotumwa na kocha mkuu Fabio Capello toka Royal Bafokeng ilipo kambi ya timu hiyo huko Afrika kusini.
Itakumbukwa kuwa Dawson ni mmoja wa wachezaji 30 walioitwa na kocha huyo wa kimataifa toka nchini Italia kabla ya kupunguzwa na kusalia wachezaji 23.
No comments:
Post a Comment